Azam FC yaivaa Mlandege akili yote ubingwa Kombe la Mapinduzi

Monday January 6 2020

Mwanaspoti-Azam FC-Tanzania- Zanzabira-yaivaa-Mlandege-akili yote-ubingwa-Kombe la Mapinduzi

 

By Muhammed Khamis

Unguja.Mabingwa watetezi wa Kombe la Mapinduzi, Azam FC wamesema wamejipanga kuhakikisha watetea ubingwa wao msimu huu.

Azam watashuka uwanja wa Amani leo ya saa 2:15 usiku kuchuana na Mlandege ya mjini Unguja ukiwa ni mchezo wake wa kwanza.

Nahodha wa Azam, Bruce Kangwa amesema hawana muda wakupoteza wanachokiwaza ni kurudisha ubingwa tu.

Alisema mashindano hayo hayo ni muhimu kwao kama ilivyokuwa michuano yoyote hawastahiki kudharau.

“Wanafahamu ugumu wa mashindano hayo kwa mwaka huu kutokana na kuchezwa kwa mtindo wa mtoano.

‘’Kutokana na mazingira haya tutahakikisha tunaongeza bidii na umakini zaidi kutwaa tena ubingwa’’aliongezea Kangwa.

Advertisement

Naye kocha mkuu wa Mlandege, Sheha Khamis amaesema wamedhamira kubadili mtazamo wa wananchi wa Zanzibar sambamba na kuonyesha kandanda safi katika mchezo wa leo.

Ameshauri uwepo wa mazingira mazuri katika mchezo huo ambao hautaweza kumpendelea yoyote yule badala yake kila kitu kiende sawa.

Advertisement