Aguero apiga bao tatu, Pep aponda hakuna kama Messi

Monday January 13 2020

Mwanaspoti-Aguero-Tanzania- Michezo-Pep-Messi-Mwanasport-Michezo-Habari

 

London, England. Licha ya Sergio ‘Kun’ Aguero kufunga mabao matatu kocha Pep Guardiola amesema Lionel Messi ndiye mshambuliaji namba moja duniani.

Aguero alifunga mabao matatu katika mchezo wa jana usiku ambao Manchester City ilishinda 6-1 dhidi ya Aston Villa.

Guardiola alisema hakuna mchezaji wa kumpiku Messi ingawa Aguero amefanya kazi nzuri dhidi ya Aston Villa.

Kocha huyo alitoa kauli hiyo alipoulizwa nani mchezaji bora ambapo alijibu Messi akimtaja ni mshambuliaji mwenye kipaji.

Pia alipoulizwa kama Messi ni mchezaji bora namba tisa, Guardiola alijibu: “Messi ni namba 9, 10, 11, 7, 6, 5 na 4, lakini Sergio ni miongoni mwao,”alisema Guardiola.

Aguero anayetoka Argentina kama Messi, amekuwa mchezaji wa kwanza raia wa kigeni kufunga mabao mengi katika Ligi Kuu England akifunga 175. Awali rekodi hiyo ilikuwa chini ya Thierry Henry aliyefunga 175.

Advertisement

Pia, Aguero amempiku nahodha wa zamani wa England Alan Shearer kwa kufunga ‘hat-trick’ mara 12 tangu alipojiunga na Man City mwaka 2011.

“Nawapongeza wachezaji wote. Kuvunja rekodi ya mchezaji nguli kama Thierry Henry haikuja kwa kipindi kifupi, imechukua miaka,”alisema Guardiola.

Advertisement