Kocha JKT Queens ataka wachezaji wake kujitambua

Thursday March 26 2020

Mwanaspoti, Tanzania, Kocha JKT Queens, Kisaikolojia kuwafundisha, soka la wanawake, wachezaji wake kujitambua

 

By OLIPA ASSA

Dar es Salaam. Kocha wa JKT Queens, Ali Ali amesema si kazi rahisi kuwaelekeza wanasoka wa kike kutunza viwango vyao hasa kwa kipindi cha mpito wa mlipuko wa ugonjwa wa corona.

Amesema ni wachezaji wachache ambao wanalinda viwango vyao hata wanaporejea majukumu hapati kazi ya kuanza upya mazoezi.

"Kisaikolojia kuwafundisha soka la wanawake lazima usiwe na hasira na ujue namna ya kuzungumza kwa lugha rahisi kwao, mfano mwanaume unaweza ukamkalipia akaona sawa, ila kwa dada zetu wataona unawadharau," amesema.

Ali amesema katika kipindi cha mpito kinachopitia dunia nzima amekuwa akiwa programu jinsi ya kutokuongezeka uzito na kufanya miili yao kuwa miepesi.

"Kwanza hata kimbia yao sio kama ya watoto wa kiume ndio maana lazima nitoe mazoezi yakuwafanya miili yao iwe miepesi, hilo litasaidia ligi ikianza," amesema kocha Ali.

Advertisement