Mwamnyeto wa Coastal Union ameingia chimbo kujifua

Muktasari:

Soka ni kazi yangu, sijalazimishwa na mtu kuifanya ndio maana kuna ulazima wa kufanya mazoezi kuwa sehemu ya maisha yangu

Dar es Salaam. Beki wa Coastal Union, Bakari Mwamnyeto amesema hatakubali kiwango chake kushuka licha ya uwepo wa mtikisiko wa ugonjwa wa corona ulisababisha ligi zote kusimama.

Amesema kila siku amepanga programu ya mazoezi kama kama alivyokuwa na timu, lengo lake likiwa nikulinda kiwango chake.

"Soka ni kazi yangu, sijalazimishwa na mtu kuifanya ndio maana kuna ulazima wa kufanya mazoezi kuwa sehemu ya maisha yangu."

"Ninachokifanya ni kwa ajili ya kulinda kiwango changu, sitaki kuwa mzigo kwa kocha Ligi itakapoanza," amasema.

Amesema si wakati wa wachezaji kula bata bali wanatakiwa kujituma zaidi ili kuweza kuhimili kipindi cha mpito wa ugonjwa wa corona.

"Kuna kipindi ambacho wachezaji wakimaliza ligi angalau mnapata muda wa kukaa ama kutembelea ndugu na jamaa ila wakati huu ni wakujitoa zaidi kupambana kulinda uwezo," amesema Mwamnyeto.