Mwambusi: Carlinhos bado

KOCHA Msaidizi wa Yanga, Juma Mwambusi amesena licha ya kwamba mashabiki wengi wanaona kama winga wao Carlos Fernandes ‘Carlinhos’ amekuwa bora, lakini yeye kwa upande wake anaona mchezaji huyo hajafika katika kiwango hicho.

“Carlinhos ni mchezaji mzuri, lakini bado anatakiwa apate mechi ‘fitinesi’, hapaswi kuwa mchezaji wa faulo na vitu vingine na akiwa fiti basi ndio tutajua,” alisema Mwambusi.

Akizungumzia kuhusu namna ya uchezaji wa kikosi chake kubadilika, alisema hilo lipo na baada ya wiki mbili kutakuwa na vitu vingi tofauti zaidi.

“Kikubwa ambacho tulikuwa tunafanyia kazi ni kuona wachezaji wakiweza kumaliza dakika 90 mpaka 120 na hilo nimeliona limeanza kujitokeza katika kikosi changu,” alisema kocha huyo wa zamani wa Mbeya City.