Mwakinyo bondia wa 68 Afrika, apanda nchini

Wednesday September 16 2020

 

By Imani Makongoro

BAADA ya kupanda wa nafasi moja nchini, Hassan Mwakinyo ametajwa kuwa bondia wa 68 Afrika katika orodha ya mabondia wa kila uzani 'lb for lb'

Mwakinyo anayepigania uzani wa super welter alikuwa bondia namba tatu nchini, amepanda kwa nafasi moja na sasa anakamata namba mbili kwenye lb for lb, akiwa nyuma ya Ibrahim Class 'King Class Mawe'.

Class anayepigania uzani wa super feather ndiye namba moja nchini na wa 52 Afrika.

Aliyekuwa bondia namba mbili nchini, Tony Rashid ambaye sasa ni namba tatu amekamata nafasi ya 71 Afrika.

Ilunga Makabu anayepigania uzani wa cruiser bondia anayetumia zaidi mkono wa kushoto anayetokea Jiji la Johannesburg na mpinzani wake, Thabiso Mchunu anayetokea huko Cato Ridge, Afrika Kusini ndiyo mabondia bora Afrika.

Nafasi ya tatu inakamatwa na Richard Commey anayepigania uzani wa light raia wa Ghana anayeishi Bronx, Marekani.

Advertisement

Mwakinyo bondia maarufu nchini aliyewahi kuwa namba moja Afrika kwenye uzani wake baada ya kumchapa Sam Egginton wa Uingereza mwaka 2018 ameporomoka kwa nafasi kadhaa, licha ya kupanda nafasi moja katika viwango vya Tanzania.

Advertisement