Muziki wa Singida United wamkuna kocha

Tuesday August 7 2018

 

By Masoud Masasi

Mwanza. Kocha Msaidizi wa Singida United, Jumanne Challe amesema vijana wake sasa wapo tayari kwa Ligi Kuu Bara.

Challe alisema kwa muda waliokaa Jijini Mwanza anafurahia vijana wake wanavyomuelewa na kufuata maelekezo na kwamba anaamini ligi itakapoanza timu pinzani zitapata tabu sana.

Alisema msimu uliopita Singida ikiwa n imara yao ya kwanza kushiriki Ligi Kuu, lakini walionyesha ushindani na mafanikio, na msimu huu wamejiandaa kufanya kweli zaidi.

“Vijana wanaendelea vizuri ni wazi msimu huu timu pinzani zijipange kula vichapo tunahitaji kuonyesha ushindani, lakini kushinda kila mchezo”alisema Challe.

Kiraka Boniface Maganga alisema wachezaji watapambana kadri ya uwezo wao kuhakikisha timu inapata matokeo mazuri na kufika mbali.

 “Kwa ujumla sisi tuko vizuri na tunatarajia tutafanya makubwa zaidi, kila mmoja ana ari na morari ya kucheza soka tunashirikiana, lakini tunaelewa kinachoelezwa na kocha kwahiyo tunasubiri ligi ianze,”alisema Maganga.

 

Advertisement