Mukoko balaa, Azam chali

Mechi mbili za kirafiki zimepigwa leo Septemba 16, 2020 katika dimba la Azam Complex Chamazi ambapo Azam FC iliikaribisha Transit Camp na Yanga SC imecheza dhidi ya Mlandege FC ya Zanzibar.

Yanga wametumia vikosi viwili tofauti kwa vipindi viwili walicheza mpira wa kuumiliki na kuanzisha mashambulizi kutokea pembeni.

Yanga imeshinda mabao 2-0, la kwanza limewekwa wavuni na Waziri Junior kwa mkwaju wa penalti dakika ya 40 na la pili limefungwa na Mukoko Tonombe aliyepiga shuti kali nje ya boksi lililoenda kwenye wavu na kumshinda kipa wa Mlandege dakika ya 59 baasa ya klutengewa mpira na Sogne.

Kikosi kilichoanza Yanga kabla ya mabadiliko golini alikuwa Metacha Mnata, mabeki Kibwana Shomari, Adeyun Salehe, Said Makapu, Abdallah Ninja, viungo Fei toto, Abdulaziz Makame, Farid Mussa, Haruna Niyonzima, washambuliaji Ditram Nchimbi na Waziri Junior.

Mlandege walicheza kwa kujiamini na kushambulia kwa kushtukiza japo mashambulizi yao hayakuwa na madhara kwa lango pinzani. Kipindi cha pili Mlandege walipata kadi nyekundu baada ya Ibrahim Juma kuonyeshwa kadi mbili za njano.

Wachezaji walioingia kipindi cha pili walibadilisha mchezo wakiongozwa na Deus Kaseke, Tuisila Kisinda, Mukoko Tonombe, Michael Sarpong, Carlos Carlinhos na Zawadi Mauya huku langoni akiingia Ramdhan Kabwili.

Kabla ya mchezo huo saa 10:00 jioni Azam imeshushiwa kichapo na Transit Camp cha mabao 2-1 ambapo Mwana mfalme Dube ameongeza kibubu chake cha mabao kwa kuweka kambani bao moja. Bao la pili Transit Camp limefungwa na Damas Makwaya na la pili Abdallah Kheri akijifunga.

Raundi ya tatu ya Ligi Kuu Bata itaendelea wikiendi hii na Azam FC itasafiri kwenda Mbeya kucheza na Mbeya City jijini huku Yanga ikitua Bukoba kukipiga na Kagera Sugar Uwanja wa Kaitaba