Mtibwa Sugar yakamia kulipa kisasi kwa KCCA

Muktasari:

  • Zimebaki siku tatu Mtibwa Sugar kucheza mechi ya marudiano na KCCA ya Uganda, mchezo huo utapigwa Jumamosi ya wiki hii jijini Dar es Salaam.

Dar es Salaam. Mchezo kwao utunzwa hiki ndicho wanachokisubiria Mtibwa Sugar, kulipa kisasi dhidi ya KCCA ya Uganda iliyowafunga kwao mabao 3-0, katika mechi za muendelezo wa michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.


Mtibwa Sugar ilianza vyema mechi yake ya kwanza dhidi ya Northern Dynamo kwa kuwafunga mabao 4-1 katika Uwanja wa Azam Complex na kuwafunga bao 1-0 kwao.
Mchezo wake wa pili na KCCA, Mtibwa Sugar haikupata matokeo mazuri, safu yao ya ulinzi iliruhusu mabao 3-0, Jumamosi ya wiki hii watarudiana na Waganda hao, jijini Dar es Salaam.


Kocha wa Mtibwa Sugar, Zuber Katwila amesema kuna faida kucheza nyumbani akidai wanakuwa wanapata sapoti ya mashabiki tofauti na ugenini.


Katwila anasema matokeo ya kufungwa na KCCA hayajawakazisha tamaa kuendelea kupambania ndoto yao ya kuhakikisha wanafika mbali kwenye michuano hiyo.


"Tunawaomba mashabiki wajitokeze kwa wingi tutakapocheza na KCCA Jumamosi ya wiki hii, tutaingia Dar es Salaam siku ya Ijumaa, tutafikia hotel ya Itumbi," alisema Katwila.