Mshindi Jackpot SportPesa apewa kitita chake

Wednesday February 12 2020

Mshindi Jackpot SportPesa apewa kitita chake,MSHINDI wa Jackpot ya SportPesa, Yawssin Ridhiwan,

 

By Mwandishi wetu

MSHINDI wa Jackpot ya SportPesa, Yawssin Ridhiwan jana Jumanne alikabidhiwa kitita chake cha zaidi ya Sh437 milioni baada ya kushinda kwenye ubashiri wake wa mechi 13.

Yassin (35), mkazi wa Ubungo jijini Dar es Salaam juzi Jumatatu alitangazwa mshindi wa Jackpot ambapo sasa amekabidhiwa zawadi yake.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi SportPesa Tanzania, Abbas Tarimba alimpongeza Yassin kwa ushindi huo wakati akimkabidhi hundi yake makao makuu ya ofisi zao, Dar es Salaam.

Tarimba alisema SportPesa ni kampuni isiyobahatisha katika michezo hiyo na ndiyo maana wamekuwa namba moja nchini huku akitoa shukrani kwa Watanzania kuwafikisha hapo walipo.

“Nichukue fursa hii kumtangaza mshindi mpya wa wiki hii wa Jackpot yetu ya SportPesa,” alisema Tarimba.

“Yassin, kama SportPesa tunaamini ndoto zake zitatimia baada ya kushinda Jackpot hii baada ya kushinda mechi 13 kiukweli siyo kazi rahisi kwake.

Advertisement

“Sh437,631,320 siyo ndogo kwa Mtanzania wa kawaida, lakini kama SportPesa tunafarijika tukiona maisha ya Watanzania yakibadilika baada ya kushinda nasi, hivyo niwatake Watanzania waendelee kubashiri nasi kwani kila wiki SportPesa itakuwa ikitoa mamilioni.”

Aliongeza kuwa, “SportPesa tunatoa zawadi kwa kila mshindi wetu ambaye ameshinda bila kuangalia mazingira anayotokea ilimradi awe na umri kuanzia miaka 18.

“Tunachukua fursa hii kuwashukuru washindi wetu wa wiki hii na kuwaomba watumie vyema pesa walizojishindia kwa ajili ya kuendeleza maisha yao, pia ni faida kwa serikali ambayo kwa kupitia ushindi wake kumeinufaisha kwa kukatwa Sh87 milioni kwenye kodi.

“Kuna washindi wengine pia waliojishindia mechi 10, 11 na 12, hivyo SportPesa tunawazawadia hata wale ambao hawakufanikiwa kubashiri mechi zote 13 kwa usahihi.”

Tarimba alisema: “Lakini kikubwa kabisa ni kodi ambayo Yassin atalipa kwa mujibu wa sheria za kodi sawa na asilimia 20 ya zawadi yake ambayo itaenda serikalini moja kwa moja, ni fahari kwetu.”

Kwa upande wa Yassin, alisema alianza kubashiri takribani miezi mitano iliyopita na alipata hamasa zaidi baada ya kuona washindi wa Jackpot wa kitita cha Sh825 milioni.

“Nilianza kucheza na SportPesa miezi mitano iliyopita baada kuwaona Magabe na Kingslay wakikabidhiwa cheki yao, niliamini na kuanza kucheza,” alisema.

“Nawashukuru SportPesa kwa kubadili maisha yangu. Nimekuwa nikimiliki biashara ndogo ya kuuza vinywaji na vitafunwa ili kuendesha maisha, lakini nitafanya biashara kubwa ambayo angalau itakuwa na uwezo wa kunilipa vizuri.”

Mwakilishi wa Michezo ya Kubahatisha Kitengo cha Ilala, Haule Philip alisema: “Ushindi unaopatikana SportPesa unakuwa wa uwazi na ndio maana Yassin ambaye mshindi, umeongeza mapato ya serikali.”

Advertisement