Msanii wa Bongo Muvi Mercy afikiria kuigiza kimataifa

Muktasari:

Mercy alianza kuwa na ndoto za kuigiza tangu akiwa shule ya msingi na kitato cha kwanza alinza kuigiza kwa kiasi lakini baadaya  akiwa sekondari kidato cha pili mwaka 2010 alijikita rasmi kwenye tasnia hiyo ambayo kwa sasa inatoa ajira kwa vijana.

Dar es Salaam. Msaanii wa filamu nchini, Maria Paul maarufu Mercy Kidoti amesema ndoto yake ni kuwa mwigizaji wa kimataifa akitokea hapa nchini ili sanaa ya uigizaji ifike mbali mbali zaidi.

Mercy Kidoti ambaye ameigiza miongoni mwa filamu za ‘Maigizo’, ‘Chanuo’ na ‘Mama Mwali’ alisema ndoto zake ni kufanya kazi kimataifa ili kuhakikisha tasnia ya sanaa inasonga mbele zaidi.

Msanii huyo wa filamu aliyasema hayo wakati wa siku yake ya kuzaliwa iliyofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Hong Kong jijini Dar es Salaam  Jumapili mwishoni mwa wiki iliyopita, ambapo aliwasihi wasanii wa kike chipukizi nchini kuhakikisha wanazikabili changamoto mbalimbali kwenye kazi yao ili kulinda heshima yao kwenye jamii.

Alisema licha ya kuipenda kazi hiyo kuna changamoto ambazo huwa zinawakabili wanawake ikiwa ni pamoja na masuala ya mapenzi kujitokeza kwenye kazi, lakini amesisitiza jambo hilo kwake sio kikwazo kutokana na kutambua na kuthamini kazi hiyo ya sanaa.

Mercy Kidoti alisema alianza kuwa na ndoto za kuigiza tangu akiwa shule ya msingi na kitato cha kwanza alinza kuigiza kwa kiasi lakini baadaya  akiwa sekondari kidato cha pili mwaka 2010 alijikita rasmi kwenye tasnia hiyo ambayo kwa sasa inatoa ajira kwa vijana.

Msanii huyo alisema alirudi kwa kishindo na kufanya  kazi hiyo mwaka jana mwezi Julai 2017, ambapo walifanya kazi ya ‘Chanuo’ na kumuweka kwenye ramani ya filamu nchini, huku tayari akiwa amefanya kazi nyingine ambazo zinafanya vizuri sokoni kama vile Mama Mwali.