Mkwasa baada ya miaka 14

Muktasari:

Mzawa wa mwisho kuinoa Yanga kabla ya Mkwasa kuteuliwa hivi karibuni, alikuwa Kennedy Mwaisabula 'Mzazi' na baada ya hapo ilikuwa ingia toka ya makocha wa kigeni kama orodha iliyopo hapo chini;

BONIFACE Mkwasa 'Master' jioni ya leo atakuwa na kibarua cha kwanza kama Kaimu Kocha Mkuu wa Yanga wakati chama lake litakapokabiliana na wenyeji wao, Ndanda FC katika mechi ya Ligi Kuu Bara itakayipigwa Uwanja wa Nangwanda Sijaoni, mjini Mtwara.
Mkwasa ameteuliwa na uongozi wa Yanga baada ya klabu hiyo kuachana na aliyekuwa Kocha Mkuu wao, Mwinyi Zahera, ikiwa ni siku chache tangu timu hiyo itolewe kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika hatua ya mtoano kuwania kutinga makundi.
Nyota huyo wa zamani wa kimataifa wa Tanzania aliyewahi kutamba na klabu kadhaa ikiwamo Yanga na Taifa Stars, anarejea klabuni hapo baada ya kujiuzulu Ukatibu Mkuu miaka miwili iliyopita kwa sababu ya kiafya.
Lakini pia anarejea Jangwani ikiwa ni miaka 18 tangu alipoifundisha timu hiyo kwa mara ya mwisho mwaka 2001.
Usichokijua labda ni hiki. Mkwasa anakuwa kocha wa kwanza mzawa kuinoa Yanga tyangu mwaka 2005, ikiwa na maana baada ya miaka 14 ndipo klabu hiyo inampa jukumu mzawa, japo ni kwa muda kwani kwa sasa mchakato wa kupata Kocha Mkuu mpya kutoka nje ya nchi unaendelea.
Miongoni mwa majina ya makocha wanaotajwa pengine kuja kuziba nafasi ya Zahera ni Hans Pluijm, Ernie Brandts wote kutoma Uholanzi, Raoul Shungu kutoka DR Congo na Kim Poulsen aliyekuwa kuwa Kocha Mkuu wa timu za taifa za vijana na Taifa Stars anayetokea Denmark.
Mzawa wa mwisho kuinoa Yanga kabla ya Mkwasa kuteuliwa hivi karibuni, alikuwa Kennedy Mwaisabula 'Mzazi' na baada ya hapo ilikuwa ingia toka ya makocha wa kigeni kama orodha iliyopo hapo chini;
2005: Kenny Mwaisabula
2006: Jack Chamangwana (Malawi)
2007: Milutin Sredojevic ‘Micho’ (Serbia)
2007: Razack Ssiwa (Kenya)
2007: Jack Chamangwana (Malawi)
2008: Dusan Kondic (Serbia)
2010: Kostadin Papic (Serbia)
2011: Sam Timbe (Uganda)
2011: Kostadin Papic (Serbia)
2012: Tom Saintfiet    (Ubelgiji)
2012-13: Ernie Brandts ( Dutch )
2013-14: Hans Van Pluijm ( Dutch )
2014: Marcio Maximo ( Brazil )
2015-2016: Hans Van Pluijm ( Dutch )
2016-2018: George Lwandamina (Zambia)
2018-2019: Zahera Mwinyi (DR Congo)
2019- Boniface Mkwasa(kaimu)