Mertens apiga bao la 121, Napoli ikilazimishwa sare na Barcelona

Muktasari:

FC Barcelona ili kumaliza pungufu kutokana na kiungo wao, Arturo Vidal kuonyeshwa kadi nyekundu muda mchache kabla ya mchezo kumalizika.

Milan, Italia. Bao la Dries Mertens alilofunga kipindi cha kwanza katika hatua ya mtoano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya FC Barcelona limemfanya kuwa mfungaji bora wa muda wote wa Napoli sawa na Marek Hamsik wakiwa na mabao 121.

Katika mchezo huo ambao ulichezwa Italia, ulimalizika kwa sare ya bao 1-1, FC Barcelona walisawazisha kipindi cha pili kupitia kwa Antoine Griezmann baada ya kupigiwa krosi na Nelson Semedo.

FC Barcelona ili kumaliza pungufu kutokana na kiungo wao, Arturo Vidal kuonyeshwa kadi nyekundu muda mchache kabla ya mchezo kumalizika.

Katika dakika ya 89, alimchezea vibaya Fabian Ruiz, lakini baada ya mchezaji huyo wa Napoli kuonyesha kuchukizwa na kitendo kile, Vidal alisogezea kichwa chake usoni kwa mwenzake na kumgonga.

Alionyeshwa kadi mbili za njano katika tukio hilo la haraka na kusindikizwa na nyekundu.

Katika mchezo wa marudiano ambao utachezwa Nou Camp, Jumatano ya Machi, 18, FC Barcelona watamkosa Vidal na Sergio Busquets atakayekuwa anatumikia adhabu ya kuonyeshwa kadi mbili za njano katika michezo miwili mfululizo.

Kocha wa Napoli, Gennaro Gattuso alisema kosa moja limewagharimu, hawakuwa hatari kwetu, ametumia kosa moja kupata bao.

Upande wake nahodha wa Napoli, Lorenzo Insigne alisema, "Tulistahili ushindi, lakini kwa aina ya matokeo yuliyoyapata yametuumiza."

Pamoja na kumiliki mpira kwa asilimia 67%, Barcelona walipiga mashuti mawili tu yaliyolenga lango la Napoli kwa dakika zote 90 za mchezo.

"Matokeo sio mabaya kwa kuzingatia tunamchezo mwingine mbele yetu wa marudiano," alisema kocha wa FC Barcelona, Quique Setien.