Mchawi Mweusi aukataa mzimu wa Serengeti Boys

Saturday November 16 2019

Mchawi -Mweusi -aukataa -mzimu - Serengeti -Boys-mashindano - Afcon- Kocha -Bakari

 

By Doris Maliyaga

KILE kilichowaumiza wachezaji wa timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 17 'Serengeti Boys' kung'olewa hatua ya mwanzo kabisa kwenye mashindano ya Afcon, Kocha Bakari Shime 'Mchawi Mweusi' amekikataa kabisa.
Shime ambaye anaifundisha timu ya taifa ya soka ya Wanawake ya Tanzania Bara 'Kilimanjaro Queens' alisema analijua hilo amejipanga baada ya kujifunza makosa.
"Ipo hiyo lakini kwangu mimi ninachohesabia ni fainali na kichukua kombe, tunashiriki na tutashinda mengine hakuna," alisema Shime.
Serengeti Boys ambao walikuwa wenyeji waliaga mapema michuano ya Afcon hatua ya makundi, ingawa mpaka wanakwenda kushiriki fainali hizo,  walikuwa na rekodi nzuri katika mashindabo tofauti ikiwemo Cosafa.
Kilimanjaro Queens inaanza kucheza karata ya kwanza leo Jumamosi dhidi ya Sudan Kusini Uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam huku ikipangwa Kundi A pamoja na Burundi,  Sudan Kusini na Zanzibar.

Advertisement