Mastraika hawa watatikisa dirisha la usajili Bongo

Saturday November 16 2019

Mastraika-a watatikisa- dirisha - usajili -Bongo-mashindano - Shirikisho - Soka- Duniani

 

LIGI Kuu ya Vodacom imesimama kwa muda kupisha kalenda ya mashindano ya Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) ambapo kwa Afrika kuna mechi za kuwania kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika (Afcon) zitakazofanyika Cameroon, mwaka 2021.

Hadi wakati Ligi hiyo inasimama, Simba inaongoza msimamo ikiwa imekusanya jumla ya pointi 22 ikifuatiwa na Kagera Sugar ambayo ina pointi 20 na Prisons inashika nafasi ya tatu ikiwa imekusanya pointi 16. Wakati huohuo Singida United inashika mkia ikiwa imekusanya pointi nne tu, nafasi ya 19 kuna timu ya Ndanda na pointi zao saba na waliopo katika nafasi ya 18 ni Mbeya City walio na pointi nane.

Baada ya kalenda ya kimataifa kupita, ligi itaendelea tena ambapo kutachezwa raundi takribani mbili na baada ya hapo itasimama tena ili kupisha mashindano ya soka ya Chalenji yanayoshirikisha nchi zinazounda Baraza la Vyma vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (Cecafa) ambayo yataanza Disemba Mosi huko Uganda.

Ni katika kipindi hicho cha kusimama kwa ligi kwa ajili ya mashindano ya Chalenji, ndipo kutafunguliwa dirisha dogo la usajili kuanzia Disemba 15 hadi Januari 16.

Kwa utangulizi, dirisha dogo la usajili limewekwa ili kuzipa nafasi timu kufanya maboresho kwenye vikosi vyao kuzingatia na mahitaji ya makocha na benchi la ufundi.

Benchi la ufundi linakuwa na fursa ya kuongeza au kupunguza wachezaji kulingana na namna lilivyofanya ‘analysis’ (tathmini) katika mechi ambazo timu husika imeshacheza.

Advertisement

Na kwa vile msimu unakuwa unaendelea, kumekuwa hakuna usajili wa idadi kubwa ya wachezaji ambao hufanyika na badala yake timu usajili au kuacha wachezaji wachache tu.

Kwa hapa Tanzania, idara ambayo imekuwa ikilegalega mara kwa mara ni ile ya

ushambuliaji hivyo kuna dalili za wazi kwamba wachezaji wanaocheza nafasi ya ushambuliaji ndio watawindwa kwa wingi kulinganisha na wale wanaocheza katika nafasi nyingine. Kwa muktadha huo, wapo washambuliaji watano ambao hapana shaka kwamba kila timu inayoshiriki Ligi Kuu, itakuwa inamtamani mmoja wao au wote kutokana na kiwango ambacho wamekuwa wakionyesha. Katika hao wachezaji sita, wapo ambao timu zinaweza kujipanga na kuwasajili kirahisi lakini kuna wengine ambao inaonekana ni ndoto za alinacha kuwang’oa katika klabu wanazocheza kwa sasa.

Meddie Kagere-Simba

Ni mchezaji aliyezaliwa kwa ajili ya kufunga na ana ujasiri wa kupambana na mabeki wa timu pinzani. Washambuliaji wa aina hiyo huwa tunawaita ‘Bull Strikers. Hadi sasa ameshapachika mabao nane.

Karibia kila timu inatamani kuwa na Kagere lakini inaonekana wazi hakuna inayoweza kumchomoa ndani ya kikosi cha Simba kwa sababu analipwa na kuhudumiwa vizuri. Ni mchezaji ambaye hana mambo mengi ndani ya uwanja, na ukiangalia namna Simba ilivyo na ‘financial muscles’ (misuli ya kiuchumi) pamoja na mtendaji mkuu (CEO) ambaye ana kiu ya kuleta mabadiliko, sidhani kama kuna timu ya hapa Tanzania inayoweza kumchukua Kagere.

Miraji Athuman-Simba

Baada ya kuvuka kutoka Lipuli kwenda Simba, mazingira yanaonekana kumbadilisha. Ndio alikuwa mchezaji mzuri na alishawahi kuifunga Yanga kabla ya kutua Simba, sasa hivi amekuwa moto wa kuotea mbali

Amekuwa akipata ‘service’ (huduma) nzuri ambayo inamfanya awe bora zaidi na amekuwa ‘akideliver’ (akitimiza) kile kinachotegemewa.

Paul Nonga-Lipuli

Kutokana na jinsi alivyotulia pale Lipuli na kutengeneza safu kali ya ushambuliaji na mwenzake Daruwesh Saliboko, Nonga amekuwa akifanya vizuri na anaisaidia vilivyo timu yake ambayo tayari ameshaifungia mabao sita katika Ligi Kuu.

Yusuph Mhilu-Kagera Sugar

Ni mchezaji mwenye kasi (speed), ‘fighting spirit’ (moyo wa kupambana), na ana ‘courage’ (jasiri). Kitendo cha kuchezea Yanga kimemfanya awe na uzoefu na kiasili ni ‘sprinter’ (anakimbia kwa kasi), kigezo ambacho mawakala wengi ndio hukitazama kwanza kwa wachezaji wanaocheza nafasi ya ushambuliaji.

Ayoub Lyanga-Coastal Union

Ni mchezaji ambaye yuko ‘strategic’ (ana mipango), mnyumbufu ndani ya eneo la hatari na ana uwezo mkubwa wa kucheza ‘far and near penalty box’ (mbali na karibu na eneo la boksi la penati.

Ditram Nchimbi-Polisi Tanzania

Huyu anajua kukaa katika nafasi. Yuko ‘very sharp’ na anaendana na ‘rythm na movement’ ya mpira na ana mwili mkubwa ambao hata hivyo amekuwa aakiutumia vizuri kwa sababu ana ‘dynamic balance’ na kingine ni kwamba ni mchezaji ambaye anarisk na haogopi kupenya katika msitu wa mabeki.

Lakini nitumie fursa hii kutoa angalizo kwa wachezaji ambalo ni wanapaswa kuwa watulivu katika kuamua na kabla hawajachagua wapi pa kwenda, wanatakiwa kujievvaluate na kujifanyia analysis ili wasipoteze viwango vyao.

Advertisement