Mashabiki Simba wawageuzia kibao wachezaji, kocha Aussems

Muktasari:

  • Mashabiki wa Simba hawakuwa na shamrashamra kama ilivyozoeleka huku wengine wakionekana kuwa na wasiwasi na kupata matokeo dhidi ya Kagera ambayo tayari iliwafunga  mzunguko wa kwanza mabao 2-1 Uwanja Kaita  Kagera.

PENGINGE kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha jijini Dar es Salaam ndizo zilizofanya mashabiki wa Simba washindwe kufika kwa wingi, kuisapoti timu yao  inayocheza na Kagera Sugar.

Simba ndio inaongoza ligi kwa pointi 81 ili kuendeleza rekodi hiyo, inategemeana na matokeo yao  na Kagera Sugar, pia mchezo wa Yanga Biashara ndiyo itakayotoa taswira ya nani ataendelea kukalia usukani wa Ligi Kuu.

Mashabiki wa Simba hawakuwa na shamrashamra kama ilivyozoeleka huku wengine wakionekana kuwa na wasiwasi na kupata matokeo dhidi ya Kagera ambayo tayari iliwafunga  mzunguko wa kwanza mabao 2-1 Uwanja Kaita  Kagera.

Jambo lingine linalowafanya mashabiki kushindwa kuishangilia timu yao ni aina ya mchezo ambao wanacheza wao ambao wanajikuta wanaiga staili ya Kagera Sugar.

Simba  wamezoeleka kucheza mpira wa kasi, lakini katika mechi hiyo wanajikuta wanacheza wa kupozeshwa ambao wanacheza Kagera Sugar.

Minong'ono ya mashabiki wa Simba wanadai kwamba Kagera ilitua jijini Dar es Salaam , wakati timu yao ipo Mbeya kucheza na Prisons ambayo waliifunga bao 1-0 Uwanja wa Sokoine, kwamba Yanga walikuwa nyuma yao.

Mbali na malalamiko yao ya kuona Yanga ipo nyuma ya Kagera, pia uwanja wa Uhuru unaonekana kuwa changamoto kwa wachezaji kutokana na unavyoteleza.

Changamoto ya Uwanja wa Uhuru kuteleza baadhi yao wanaiona huku wengine wakiona wachezaji wao wazembe na kucheza mpira wa kupozwa wa Kagera Sugar.

Bao ambalo Simba wamejifunga kupitia kwa beki wao Mohamed Hussein 'Tshabalala' lilitibua mambo kwa mashabiki ambao walianza kutukana na baadhi kujikuta wakijikuta wanatengua udhu.

Mbali na kukerwa na wachezaji pia kocha wa Simba, Patrick Aussems amejikuta kwenye wakati mgumu kwa mashabiki wake wakidai kwamba anapanga kikosi ambacho sio cha ushindi.