Martinez awaaga mashabiki Arsenal

Thursday September 17 2020

 

London, England. Kipa Emiliano Martinez ametuma ujumbe wa kuaga mashabiki wa Arsenal akithibitisha kuondoka katika klabu hiyo kwa kitita cha Pauni 20 milioni kujiunga na Aston Villa.

Shujaa huyo wa meechi ya fainali ya Kombe la FA hakutaka kuondoka kinyonge kwa kushindwa kucheza kwenye kikosi cha sasa, akiwa kama kipa wa muda mrefu wa Gunners.

Martinez raia wa Argentina alikamilisha vipimo vyake vya afya na kukubali kusaini mkataba wa miaka minne kuitumikia Villa, huku akikubali mshahara wa Pauni 60,000 kwa wiki.

Katika ujumbe wake kwenye mtandao wa Instagram, kipa huyo mwe miaka 28 alithibitiosha kuondoka na kuwa mwenye furaha kuondoka Emirates, baada ya kukasirishwa na kutakiwa kutolewa kwa mkopo.

Baada ya kuisaidia Arsenal kuichapa Chelsea mabao 2-1 katika mchezo wa fainali ya Kombe la FA, alirudi Wembley kuisaidia tena miamba hiyo ya London kutwaa Ngao yua Jamii mbele ya Liverpool.

Martinez alisema “Nina furaha sana kuwepo Arsenal kwa miaka 11, licha ya kuwa ilikuwa ni kazi ngumu kwa miaka yote hiyo kwangu.”

Advertisement

 

Advertisement