Man United msimu ujao usipime

Muktasari:

Kocha Ole Gunnar Solskjaer anataka kikosi chake kiundwe na wachezaji vijana ili watumike kwa muda mrefu.

LONDON,ENGLAND . MANCHESTER United tayari imeshaanza kuufanyia kazi mpango wake wa kufanya usajili mkubwa katika dirisha la majira ya kiangazi mwaka huu ya kuwaweka Jack Grealish, James Maddison na Jadon Sancho kwenye orodha ya mastaa inaotaka kuwasajili.

Makamu mwenyekiti mtendaji wa klabu hiyo, Ed Woodward ametangaza wazi Man United itamwaga pesa kutengeneza kikosi chake kuwa kwenye ubora mkubwa.

Tayari timu hiyo imeshafanya usajili wa mastaa watano kutengeneza kikosi hicho akiwamo Daniel James, Aaron Wan-Bissaka, Harry Maguire, Bruno Fernandes na Odion Ighalo, ambaye anapita tu na mkopo wake utakapokwisha ataondoka.

Kocha Ole Gunnar Solskjaer anataka kikosi chake kiundwe na wachezaji vijana ili watumike kwa muda mrefu.

Kama itawapata mastaa hao watatu, Grealish, Maddison na Jadon Sancho basi kikosi cha Man United kwa msimu ujao kitakuwa balaa kubwa.

Golini kama kawaida atakuwa David de Gea, ambaye atalindwa na ukuta wa mabeki Aaron Wan-Bissaka upande wa kulia, Victor Lindelof na Harry Maguire watacheza beki ya kati na kushoto atacheza Brandon Williams.

Kikosi hicho kitakachotumia fomesheni ya 4-3-3, katikati, kiungo mkabaji atakuwa Scott McTominay, akisaidiana na viungo wengine wa kati, Bruno Fernandes na Jack Grealish huku Paul Pogba akiondolewa kabisa kwenye kikosi.

Kwenye fowadi, wingi ya kulia atakuwa Sancho, kushoto ni Rashford na straika ni Moussa Dembele.

Kikosi cheki picha.