Man United kwa Wolves, Man City vitani na Swansea robo fainali FA

Muktasari:

  • Pia hatua hiyo ya robo fainali itazikutanisha Swansea v Man City, Watford Crystal Palace, Millwall v Brighton ambapo mechi zote zitachezwa weekend ya Machi 16-17.

England. Ushindi wa Manchester United dhidi ya Chelsea kwenye dimba la Stamford Bridge umewapeleka Mashetani Wekundu hatua ya robo fainali mechi ambayo watakutana na Wolves.

Mabao ya Manchester United yaliwekwa wavuni na Ander Herrerra pamoja a na Paul Pogba aliyewegongelea msumari wa mwisho jana Jumatatu usiku.

Kocha wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer ameendelea kujitengenezea mazingira ya kuwa kocha wa kudumu klabu hapo kutokana na ushindi huo mnono alioupata jana.

Hata hivyo, upande wa Chelsea mambo yanaonekana kuwa mabaya zaidi kwa kocha Maurizo Sarri ambaye  amekuwa na wakati mgumu klabu hapo kutokana na kutofanya vyema huku mashabiki wakichukizwa na mwendelezo wa matokeo mabaya.

Pia hatua hiyo ya robo fainali itazikutanisha Swansea v Man City, Watford Crystal Palace, Millwall v Brighton ambapo mechi zote zitachezwa weekend ya Machi 16-17.

Vikosi vilivyocheza jana, Chelsea: Arrizabalaga; Azpilicueta (Zappacosta 82), Rudiger, David Luiz, Alonso; Kante, Jorginho, Kovacic (Barkley 71); Pedro (Willian 58), Higuain, Hazard

Hawa hawakutumia: Caballero, Giroud, Hudson-Odoi, Christensen

Kikosi cha Man United kilichocheza jana: Romero; Young, Smalling, Lindelof, Shaw; Herrera, Matic, Pogba; Mata (Pereira 76); Rashford (McTominay 90), Lukaku (Sanchez 73)

Hawa hawakuanza: De Gea, Bailly, Fred, Dalot