Man United kuipiga bao Real Madrid kwa straika Haaland

Muktasari:

Upinzani mkubwa upo kwa klabu ya Real Madrid ambao wanaonekana kuwa wanaihitaji saini ya straika huyo kwa udi na uvumba. Lakini United wanaoneka kuwa mbele zaidi kwenye mbio hizo.

MANCHSTER United inajiandaa kutoa jumla ya Pauni 63 milioni ili kumvuta straika wa klabu ya Borussia Dortmund, Erling Haaland katika dirisha lijalo la majira kiangazi. Kiasi hicho ndicho ambacho kipo kwenye kipengele cha mkataba wa mchezaji huyo iwapo kuna timu itahitaji kumchukua.

Upinzani mkubwa upo kwa klabu ya Real Madrid ambao wanaonekana kuwa wanaihitaji saini ya straika huyo kwa udi na uvumba. Lakini United wanaoneka kuwa mbele zaidi kwenye mbio hizo.

Haaland mwenyewe aliweka wazi kuwa anatamani kubakia kwenye kikosi cha Dortmund walau kwa msimu mmoja zaidi. Straika huyo alijiunga na miamba hiyo ya Ujerumani katika dirisha dogo la Januari kwa ada ya uhamisho ya bei ya mbuzi Pauni 18 milioni, usajili wake unatajwa kuwa moja ya sajili zitakazosumbua sana katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi kama atauzwa.