Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Makocha wamiminika kuomba kazi KMC

Muktasari:

Sitta alisema siku chache baada ya kuachana na Mayanja anayeinoa kwa sasa Klabu ya Kyetume FC inayoshiriki Ligi Kuu Uganda iliyopo nafasi ya 12 kwenye msimamo wa ligi hiyo yenye timu 16 hawakuwa na presha ya kumtafuta kocha mpya kwa sasa.

KMC wanaendelea na mazoezi yao jijini Dar es Salaam kujiandaa na mechi zake za Kombe la FA pamoja na Ligi Kuu Bara, lakini unaambiwa mezani kwa mabosi wa klabu hiyo kuna maombi ya kazi ya makocha kadhaa wakitaka kurithi nafasi ya Jackson Mayanja aliyetimuliwa hivi karibuni.
Mwenyekiti wa KMC, Benjamin Sitta amesema idadi ya maombi ya makocha wanaoomba kazi kwenye timu hiyo imezidi kuongezeka kila kukicha wakitaka kufanya nao kazi.

Sitta alisema siku chache baada ya kuachana na Mayanja anayeinoa kwa sasa Klabu ya Kyetume FC inayoshiriki Ligi Kuu Uganda iliyopo nafasi ya 12 kwenye msimamo wa ligi hiyo yenye timu 16 hawakuwa na presha ya kumtafuta kocha mpya kwa sasa.

Alisema makocha wengi wameonyesha nia ya kufanya kazi nao, lakini hilo haliwapi presha ya kuharakisha kufanya hivyo kwani kuna vitu ambavyo vimewekwa kipaumbele kwa upande wao kwa muda huu.

"Kukimbilia kumchukua kocha halafu tukaanza kujuta hilo ndio hatutaki litutokee, tumetulia na mwisho tutamchukua kocha kulingana na mahitaji ambayo yapo kwenye timu.

"Kwa sasa nipo nje ya ofisi hivyo sitaweza kukupa idadi kamili ya waliotuma maombi, lakini wapo wazawa na wengine kutoka nje ya nchi kama vile Uarabuni wote wameomba," alisema Sitta.

Kuhusu usajili wa wachezaji wapya dirisha dogo la wachezaji, alisema hilo halipo kwenye hesabu zao kwa sasa kutokana na wachezaji wengi waliokuwa majeruhi kurejea kikosini na kuanza mazoezi.

"Bajeti yetu hairuhusu kwa sasa kufanya hivyo, tuna wachezaji wa kutosha na hakuna mchezaji ambaye ataachwa zaidi ya kutolewa kwa mkopo kama itaruhusu kufanya hivyo." amesema Sitta

Kwa sasa KMC  ipo chini ya Hamad Ali akiendesha gurudumu baada ya kuondoka kwa Mayanja ambaye alipokea mikoba ya Etienne Ndayiragije aliyetimkia Azam FC na sasa anakinoa kikosi cha Taifa Stars.