Makocha 108 waomba kumrithi Aussems Simba

Muktasari:

Idadi hiyo yote inasaka nafasi ya kurithi mikoba ya Patrick Aussems aliyetimuliwa hivi karibuni.

Dar es Salaam.Baada ya Simba kutangaza kuachana na kocha wao, Patrick Aussems inaelezwa makocha 108 wameomba kazi ya kuifundisha timu hiyo.

Akizungumza katika redio Wasafi FM, Afisa Habari wa Simba, Haji Manara akiwa na Mkurugenzi wa Wanachama, Hashimu Mbaga alisema idaidi ya makocha waliomba kazi ya kuifundisha Simba imefika 108.

"Idadi ya makocha waliiomba nafasi ya kukifundisha kikosi chetu ni kubwa sana, lakini hatuwezi kusema haya."

Mbaga alisema pia katika upande mwingine wa mkutano wao mkuu utakaofanyika Jumapili, alisema kila kitu kinaenda sawa kuelekea mkutano huo.

"Usalama na vitu vingine vipo sawa kabisa, tunatarajia mpaka saa sita tutakuwa tumemaliza kila kitu kama ratiba ikienda vizuri," alisema Mbaga.