Majeruhi walivyopiga timu za Ligi Kuu England

Muktasari:
Man United yenyewe ilitumia Pauni 25.7 milioni kulipa mishahara ya wachezaji waliokuwa majeruhi, huku staa wao Alexis Sanchez akitumia pesa nyingi, Pauni 6.25 milioni alizolipwa alipokuwa mgonjwa kwenye chumba cha madaktari huko.
LONDON,ENGLAND .MANCHESTER United na Manchester City zimelipa zaidi ya Pauni 50 milioni za jumla kwa wachezaji wao majeruhi msimu uliopita.
Man City ya Pep Guardiola ilikuwa na bahati mbaya ya majeruhi msimu uliopita, lakini walifanya kweli kuwapiku Liverpool kwenye mbio za ubingwa wa Ligi Kuu England.
Kwa mujibu wa Daily Mail, Man City iligharimika pesa nyingi sana kwa wachezaji majeruhi.
Kulikuwa na majeruhi 35 tofauti na hayo yamewagharimu Pauni 24.95 milioni.
Staa wao Mbelgiji, Kevin De Bruyne, anayelipwa mshahara wa Pauni 350,000 kwa wiki, alipata majeruhi matano tofauti na kumfanya akae nje ya uwanja kwa muda mrefu, huku Man City ikitumia Pauni 8.4 milioni kumlipa mshahara huyo akiwa kwenye chumba cha matibabu.
Man United yenyewe ilitumia Pauni 25.7 milioni kulipa mishahara ya wachezaji waliokuwa majeruhi, huku staa wao Alexis Sanchez akitumia pesa nyingi, Pauni 6.25 milioni alizolipwa alipokuwa mgonjwa kwenye chumba cha madaktari huko.
Cheki hapa mishahara iliyolipwa na timu za Ligi Kuu England kwa wachezaji wao wagonjwa katika kipindi ambacho hawakucheza kwenye ligi hiyo msimu uliopita.