Majeruhi Nyoni kuwawahi Kenya

Monday June 24 2019

 

By Khatimu Naheka

Cairo, Misri. Beki wa Tanzania, Erasto Nyoni huenda akapona haraka majeraha yake na kucheza mechi dhidi ya Kenya utakaochezwa Alhamisi Juni 27, 2019.

Nyoni amekosa mechi ya kwanza dhidi ya Senegal kutokana na kusumbuliwa na majeruhi jambo lililomlazimisha kocha Emmanuel Amunike kumwanzisha David Mwantika pamoja na Kelvin Yondani

Akizungumza hali ya Nyoni, Daktari wa Stars, Richard Yomba alisema beki huyo alipata maumivu ya mguu wakati mechi ya kirafiki dhidi ya Zimbabwe.

Yomba alisema baada ya maumivu hayo walianza haraka kumpatia matibabu maalum mkongwe huyo, lakini akashindwa kuwa sawa muda mfupi kabla ya mchezo dhidi ya Senegal.

Alisema kwa sasa wanaendelea na uangalizi pamoja na matibabu zaidi ambapo hali yake inaendelea vyema na huenda akawa sehemu ya kikosi hicho katika mchezo ujao.

Aidha Yomba alisema ukiondoa Nyoni na Aggrey hakuna mchezaji mwingine majeruhi baada ya mchezo wa juzi na kila mmoja yuko sawa kuendelea na ratiba ya makocha.

Advertisement

"Tunaimani atakuwa sawa kabla ya mechi ijayo tutaendelea kumfuatilia kwa karibu kuangalia ustahimilivu wake katika mazoezi ya siku mbili zijazo, kwa sasa anafanya mazoezi ya gym, pia anaendelea na matibabu zaidi," alisema Yomba.

Advertisement