Majanga yaendelea kuiandama Liverpool

LIVERPOOL, ENGLAND. LIVERPOOL yaendelea kianguasha pointi katika muendelezo Ligi Kuu, England baada ya leo kutoka sare ya mabao 2-2 katika mchezo wa Derby dhidi ya Everton.
 
Liverpool  ndio ilikuwa ya kwanza kupitia kwa mshambuliaji wake Sadio Mane dakika ya tatu kabla ya Everton kusawazisha dakika ya 19, kupitia kwa Michael Keane.

Liver iliandika bao la pili kupitia staa wake Mohamed Salah dakika ya 72, lakini dakika saba baadae Dominic Calvert-Lewin aliisawazishia Everton.

Huo unakuwa ni mchezo wa tano kwa Liver na imeshinda mechi tatu, sare moja na kupoteza mchezo mmoja huku ikishikilia nafasi ya pili na alama zao 10.

Liverpool ilijipatia bao la tatu kupitia kwa nahodha wao, Jordan Herdasonlakini lilikataliwa baada ya kugundulika kuwa Sadio Mane ambaye alihusika kwenye bao hilo alikuwa ameotea dakika za nyongeza baada ya 90 kumalizika


Everton ambayo haijawahi kupata ushindi mbele ya Liver katika mechi za EPL, tokea mwaka 2011, ikiwa imetoka sare mara 11 na kufungwa zote bado inashikilia nafasi ya kwanza ikiwa na alama 13.

Chelsea ikiwa Stamford Bridge nayo ikabanwa mbavu na Southampton baada ya kutoka sare ya mabao 3-3, mabao yao yakifungwa na mshambuliaji wao mpya Timo Werner aliyeingia kambani mara mbili huku Kai Havertz naye akifunga bao la tatu.

Mabao ya Southampton yalifungwa na Danny Ings, Che Adams na Jannik Vestergaard, baada ya matokeo hato Chelsea imepanda hadi nafasi ya sita ikiwa na alama nane, huku Soton nayo ikipanda hadi nafasi ya 10 ikiwa na pointi saba.