Lulu avishwa pete na Majizo

Monday October 1 2018

 

By Rhobi Chacha

Dar es Salaam. Msanii wa filamu za kibongo anayetingisha kwenye fani hiyo, Elizabeth Michael ‘Lulu’,  jana Jumapili ya Septemba 30, 2018,  ilikuwa nzuri baada ya kuvalishwa pete na mchumba wake wa siku nyingi Francis Shiza ‘Majizo’.

Tukio hilo limefanyika katika sherehe ya wadogo wa mrembo huyo, ndipo CEO huyo wa EFM, alipoamua kutumia nafasi hiyo kwa ajili ya kumvisha pete mwigizaji huyo wa filamu ambaye alikuwa kimya kwa muda mrefu.

Lulu, alihukumiwa kifungo baada ya kukutwa na hatia na kusabisha kifo cha mwigizaji nguli wa filamu hizo,  Steve Charles  Kanumba.

Akiongea muda mchache baada ya kuvalishwa pete, Lulu ambaye alionekana kuwa na furaha iliyopitiliza huku akitoa maneno machache kwa mchumba wake huyo.

“Nashukuru kwa kunichagua, nakupenda, sina mengi ya kuongea zaidi ya hayo,” alisema Lulu kupitia Cheni TV.

Hata hivyo kuna madai ya kuwa ndoa ya Majizo na Lulu itakwenda kufanyika Dubai mwezi Novemba na baada ya hapo watarudi Tanzania kwa ajili ya kufanya sherehe ambayo itahudhuriwa na watu wake wa karibu.

 

Advertisement