Luiz awaibukia Lacazette, Aubameyang

Muktasari:

Mchezaji huyo raia wa Brazil alijiunga na kambi ya Emiratea akitokea Stamford Bridge kwa ada ya Pauni 8 milioni

London, England.NYOTA mpya wa Arsenal, David Luiz says amesema kuwa anajiona mwenye bahati kubwa kucheza pamoja na Alexandre Lacazette na Pierre-Emerick Aubameyang.

Mchezaji huyo raia wa Brazil alijiunga na kambi ya Emiratea akitokea Stamford Bridge kwa ada ya Pauni 8 milioni katika siku ya mwisho ya dirisha la usajili na sasa amejiunga na Unai Emery, ambaye amewahi kumnoa akiwa katika klabu ya PSG.

Mechi ya mwisho ya kimashindano ya mchezaji huyo ilikuwa ya fainali ya Ligi ya Europa dhidi ya Arsenal ambapo Chelsea iliibuka na ushindi mnono wa mabao 4-1.

Baada ya kusaini mkataba wa miaka miwili pale Arsenal, mchezaji huyo alisema kuwa anafahamu kwamba kucheza Lacazette na  Aubameyang ni faida kwake na hiyo itawaongezea ushindi.