Liverpool waambiwa mchukueni huyu Sane

Muktasari:

Na Liverpool wameambiwa wamsajili Kane na kuachana na Adama Traore wa Wolves, hayo yakiwa ni maneno ya mchezaji wa zamani wa Man City, Danny Mills.

LIVERPOOL, ENGLAND . LIVERPOOL wametakiwa kuungana na Bayern Munich kwenye mbio za kumfukuzia winga wa Manchester City, Leroy Sane ili kunasa huduma yake katika dirisha lijalo la uhamisho wa majira ya kiangazi.

Mabingwa wa soka wa Ujerumani, Bayern hawajawahi kuficha dhamira yao ya kumtaka Sane arudi kukipiga Ujerumani, huku Man City wakijiandaa kuachana na huduma ya mchezaji huyo, lakini wakihitaji mzigo wa Pauni 90 milioni.

Na Liverpool wameambiwa wamsajili Kane na kuachana na Adama Traore wa Wolves, hayo yakiwa ni maneno ya mchezaji wa zamani wa Man City, Danny Mills.

Sane alirejea mazoezini hivi karibuni baada ya kuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu alipoumia kwenye mechi ya Ngao ya Jamii baina ya Man City na Liverpool mwanzoni mwa msimu.

Kabla ya kuumia, alikuwa mchezaji muhimu kwenye kikosi cha Man City, ambapo aliwasaidia kubeba mataji saba katika kipindi cha misimu miwili, ikiwamo mataji mawili mfululizo ya Ligi Kuu England, huku akifunga mabao 39 katika mechi 134.

Na Mills naamini uzoefu wa staa huyo wa Kijerumani ni jambo la msingi kuliko kuhangaika kumsajili Traore.

“Adama Traore anapata sifa na kuandikwa kwa sababu ya nguvu zake, lakini ukihitaji mtu wa ubingwa unahitaji mtu kama Leroy Sane,” alisema Mills ambaye alikuwa staa ndani ya Liverpool.