Lacazette amtolea uvivu Wenger

Muktasari:

  • Lacazette aliyekuwa na baadhi ya wachezaji kadhaa waliouwa wakifujwa na Wenger kwa maana walisugua benchi, alimsfu kocha huyo kwa uwezo wake kusimamia majukumu ya timu.

LONDON,England.KOCHA wa zamani wa Arsenal, Arsene Wenger alitumia msuli kunasa saini ya Alexandre Lacazette kutoka Lyon hadi akamwaga wino Julai 6, 2017, lakini straika huyo juzi Jumanne amemnanga Wenger huku akimpa tano kocha wa sasa, Unai Emery.

Lacazette aliweka wazi kuwa Kocha Emery ni bonge la kocha na kuna tofauti kubwa ya utendaji kazi wa makocha hao wawili.

Wenger ametumikia Arsenal kwa miaka 22 na kuipa mataji kadhaa; ubingwa mara tatu wa EPL, ubingwa mara saba Kombe la FA kabla ya kutupiwa virago kutokana na mwenendo mbaya wa klabu.

Mabosi wa Arsenal hawakutumia nguvu nyingi kupata mbadala licha ya Wenger kumtaja mrithi wake, lakini Emery akaletwa kikosini na falsafa zake.

Lacazette aliyekuwa na baadhi ya wachezaji kadhaa waliouwa wakifujwa na Wenger kwa maana walisugua benchi, alimsfu kocha huyo kwa uwezo wake kusimamia majukumu ya timu.

Baada ya kutua Emery hapo Emirates, alipambana na sasa Arsenal iko nafasi ya nne na katika Europa League imeingia nusu fainali kwa kuitoa Napoli kwa jumla ya mabao 3-0 wiki iliyopita.

Lacazette, ambaye amepiga mabao 16 mashindano yote msimu huu, alisema: ‘Huweziamini, kuna utofauti mkubwa kati ya Emery na Wenger.