Kombe la Shirikisho... Kocha Simba amaliza mchezo

Muktasari:

Akizungumza na Mwanaspoti, Vanderbroek alisema wanaenda kuwakabili wapinzani hao bila kujali historia ya nyuma, isipokuwa kwa sasa timu hiyo inaheshimu kila mechi.

SIMBA leo inacheza dhidi ya Stand United lakini inakutana na kocha aliyewatoa kwenye Kombe la Shirikisho msimu uliopita, Atuga Manyundo.

Lakini Kocha wa Simba, Sven Vanderbroek amesisitiza kwamba rekodi hazina chochote cha kufanya kwenye mchezo wa leo, kila kitu watakimaliza kwa kutumia akili mpya ndani ya dakika 90 kwenye Uwanja wa CCM Kambarage.

Manyundo aliwafunga Simba msimu uliopita wa mashindano hayo na kuwaondoa kwenye michuano hiyo hatua ya 32-Bora akiwa na Mashujaa FC iliyowapiga Wekundu wa Msimbazi mabao 3-2, ndani ya Uwanja wa Taifa. Na sasa anakutana nayo akiwa na Stand United.

Simba inakutana na wapinzani hao wakijivunia rekodi ya ushindi katika Uwanja huo, mara ya mwisho wakikutana na kwenye mchezo wa Ligi Kuu msimu uliopita wakashinda bao 1-0 kabla ya kushuka Daraja.

Akizungumza na Mwanaspoti, Vanderbroek alisema wanaenda kuwakabili wapinzani hao bila kujali historia ya nyuma, isipokuwa kwa sasa timu hiyo inaheshimu kila mechi.

“Hatuchezi kwa rekodi na sitaki kufikiria yaliyotokea nyuma, tunawaheshimu wapinzani na tunaenda kupambana kuhakikisha tunashinda, vijana wangu wako fiti huu mchezo utaamuliwa kwa mbinu mpya za ndani ya dakika 90,” alisema Vanderbroek ambaye wimbi ya kutaka ang’oke limetulia.

Katika mazoezi ya juzi kwenye ndani ya Kirumba Mwanza, Kipa Aishi Manula, mabeki Erasto Nyoni, Shomari Kapombe, Mohammed Hussein, Luis Miquissone na nahodha wake, John Bocco hawakufanya mazoezi.

Lakini Meddie Kagere, Jonas Mkude, Paschal Wawa, Francis Kahata na Cloutus Chama walijifua kivyao.

Mazoezi ya nyota hao ilikuwa ni kukimbia uwanja mzima zaidi ya mara tano pamoja na kujinyoosha viungo kuweka mwili sawa, huku kocha wao akikomaa na wachezaji wengine.

KAGERE NA BOCCO

Benchi la ufundi la Stand United limeandaa mkakati maalumu ya kuhakikisha Meddie Kagere na John Bocco hawasababishi madhara kwao leo.

Mchezo huo wa hatua ya 16 unapigwa jioni hii ambapo

Kocha Msaidizi wa Stand, Ramadhan Mohammed alisema; “Tunajua Bocco na Kagere wako moto sana sisi kikubwa tunachofanya ni kuwafua mabeki wetu na tumekuwa tukiwapa mazoezi maalumu ya kuwabili hawa washambuliaji.”