Kocha Yanga awapunguzia dozi wachezaji

Friday August 10 2018

 

Morogoro. Kocha MKuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amewapunguzia dozi ya mazoezi wachezaji wake leo asubuhi.

Yanga tangu ifike hapa ilikuwa ikifanya mazoezi mara mbili kwa siku wakianza asubuhi na kurejea tena jioni.

Leo Zahera amewataka wachezaji wake kupumzika ambapo mazoezi yao yatafanyika kwa kipindi kimoja pekee jioni.

Hiyo inakuwa ni mara ya kwanza kwa wachezaji hao kupewa mapumziko hayo kwa kufanya mazoezi mara moja tangu wametua Morogoro

Advertisement