Kocha Mayanja atajwa kutua AFC Leopards

Muktasari:

  •  Inaelezwa kuwa kocha Matano anaondoka na kwamba chaguo jingine kwa Leopards ni Mganda George ‘Best’ Nsimbe.

Kenya. Aliyekuwa kocha msaidizi wa Simba, Jackson Mayanja, huenda akatua katika kikosi cha AFC Leopards ya Kenya.

Kutua kwa kocha huyo katika klau hiyo, pia itategemea kuondoka kwa kocha Robert Matano ambaye anaelezwa huenda akarejea katika chama lake la zamani la Tusker.

Matano aliisaidia timu yake kutwaa ubingwa mwaka 2012 na kuchukua Kombe la Nane Bora mwaka 2013. Ni msimu huu ameiongoza Ingwe kushinda taji la Ngao ya GOtv licha ya kusuasua kwenye Ligi Kuu.

Nsimbe kwa upande wake alipigwa marufuku kuongoza timu hiyo kwenye mechi tano za mwisho wa msimu naibu wake Francis Baraza akichukua hatamu kwa muda naye kocha wa kikosi hifadhi Leonard Odipo akijiunga naye kwenye benchi.