Klopp aihofia Everton ya Ancelotti

London, England. Jurgen Klopp amesema alishajua mapema kuwa Everton itakuja kuwa mshindani katika mbio za ubingwa wa Ligi Kuu England na kwa Liverpool, wakati Carlo Ancelotti alipotangazwa kuwa kocha wa miamba hiyo ya Goodison Park.

Toffees ipo katika wakati mzuri kwa sasa ikiongoza msimamo wa Ligi Kuu wakati leo ikiivaa Liverpool katika mechi ya mahasimu wa Merseyside.

Klopp hashangazwi na mafanikio ya miamba hiyo kwa sasa kutokana na kufanya usajili mzuri na kuwa na kocha bora.

“Ninachofikiri kuhusu Carlo Ancelloti wala si kitu cha siri. Namheshimu sana. Ni mtu mzuri,” kocha huyo raia wa Ujerumani aliiambia BBC Football Focus.

“Niliposikia kuwa anasaini kuifundisha Everton nikasema “Uhhh, Everton wanakuwa washindani wengine wapya’.

“Walifanya usajili mzuri msimu huu. Wamepata wachezaji sahihi wanaoweza kuimarisha timu na tayari wameanza kuwa na timu nzuri.

“Pamoja, ukichanganya na uwezo wa Carlo jinsi anavyotaka wacheze vizuri ndiyo silaha kubwa kwao.”

Kiwango bora cha Dominic Calvert-Lewin, ambaye ameshaifungia Everton mabao tisa msimu huu, ndiye mchezaji hatari kwa sasa na hali imebadilika ndani ya Goodison.

Aliongeza: “Calvert-Lewin, natarajia atapiga hatua zaidi katika miaka michache ijayo.

“Kwasasa wanafanya kazi pamoja, winga zao zote ni wachezaji wakubwakama James (Rodriguez) na Richarlison. kati kuna Allan, ukimuongeza na Sigurdsson au yeyote mwingine.