Kisa Corona Neymar, Mbappe kuzitosa Real Madrid, Barcelona

Muktasari:

Gazeti la L’Equipe limeripoti usajili wa wachezaji hao ambao wana husishwa zaidi na miamba miwili ya kule nchini Hispania, Real Madrid na Barcelona, utakuwa mgumu sana iwapo maambukizi ya Covid19 yataendela kushamiri.

Mastraika wa PSG, Kylian Mbappe na Neymar wanaweza wakabakia klabuni hapo kwa msimu huu na msimu ujao, sababu kubwa ikielezwa ni iwapo mlipuko wa virusi vya Corona utaendelea kuusakama ulimwengu wa soka.

kutokana na janga hili la virusi vya Corona athari kubwa sana itatokea kwenye soko la usajili kwa msimu ujao na hali hii inatazamiwa kuwafanya PSG kutokubali kuwaachia wachezaji hao waende katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi, wakati ligi zinatazamiwa huenda zikaanza mwezi Julai na Agosti iwapo hali itakaa sawa.

Gazeti la L’Equipe limeripoti usajili wa wachezaji hao ambao wana husishwa zaidi na miamba miwili ya kule nchini Hispania, Real Madrid na Barcelona, utakuwa mgumu sana iwapo maambukizi ya Covid19 yataendela kushamiri.

Taarifa kutoka Ufaransa zinasema PSG imeanza kuwashawishi wachezaji hao ili kuangalia uwezekano wa kuwabakisha kwa msimu huu na ripoti zinasema Mbappe ana asilimia zaidi ya 80 za kubakia klabuni hapo lakini sintofahamu ipo kwa Neymar..