Keita agonganisha vichwa mabosi wake

Muktasari:

  • Hata hivyo, Shirikisho la Mpira wa Miguu la Guinea lilipinga taarifa ya Liverpool na kudai kuwa kama nchi wana haki ya kuthibitisha afya ya nyota wao na watashikilia msimamo kuwa Keita atakuwa miongoni mwa nyota watakaoshiriki AFCON mwaka huu.

GUINEA wameendelea kuivalia njuga Liverpool juu ya kiungo wao Nabir Keita wakisisitiza kuwa atashiriki Fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON) mwaka huu huko Misri licha ya klabu hiyo kudai kuwa nyota huyo ana majeraha yanayomlazimisha kuwa nje kwa miezi miwili.

Keita alipata majeraha hayo katika mchezo wa kwanza ugenini wa hatua ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Barcelona na siku chache baadaye Liverpool walitoa taarifa ya muda atakaokaa nje ili kuuguza majeraha yake.

Hata hivyo, Shirikisho la Mpira wa Miguu la Guinea lilipinga taarifa ya Liverpool na kudai kuwa kama nchi wana haki ya kuthibitisha afya ya nyota wao na watashikilia msimamo kuwa Keita atakuwa miongoni mwa nyota watakaoshiriki AFCON mwaka huu.

Na kwa kuonyesha kuwa hawana mzaha na suala la Keita, Kocha wa Guinea, Paul Put amesisitiza kuwa Keita atashiriki AFCON.

“Amewasiliana na daktari wake huko Uswizi kama nilivyosema mwanzo. Anaendelea na matibabu. Ameanza kufanya mazoezi ya baiskeli na inatajwa kuwa atakuwa tayari kuungana na kikosi ndani ya wiki mbili na inawezekana akawemo hata kwenye kikosi cha fainali ya Ligi ya Mabingwa.