Kagere benchi Simba ikiivaa Namungo

Sunday August 2 2020

 

By Yohana Challe

Zimesalia dakika chache kabla ya mchezo wa fainali Kombe la Azam Sports Federation (ASFC) kupigwa kati ya Namungo FC na Simba leo Agosti 2, 2020.

Mchezo huo unachezwa pale Sumbawanga kwenye Uwanja wa Nelson Mandela huku Simba ikiwa ya kwanza kuanika kikosi chake.

Katika kikosi hicho Kocha, Sven Vandenbroeck amemweka benchi, Meddie Kagere ambaye ni kinara wa mabao katika Ligi Kuu msimu huu akifunga mabao 22.

Wachezaji walioanza, langoni amekaa Aishi Manula, huku safu ya ulizi akiwa, Shomari Kapombe, Mohamed Hussein, Kennedy Juma na Pascal Wawa.

Viungo ameanza, Jonas Mkude, Luis Miquissone, Gerson Fraga, na safu ya ushambuliaji akiwa, John Bocco, Clatous Chama na Francis Kahata.

Wachezaji wa akiba yupo, Kagere, Gadiel Michael, Yusuph Mlipili, Yassin Mzamiru, Deo Kanda na Hassan Dillunga.

Advertisement

Hadi leo kwenye ASFC vinara wamagoli katika timu zote mbili Chama wa Simba anaongoza kwa mabao manne na Bigirimana wa Namungo ana mabao mawili.

Kikosi Namungo; Nourdine Barola, Rogers Gabriel, Edward Manyama, Steven Duah, Karlos Protas, Hamis Khalifa, Hashim Manyanya, Daniel Joram, Bigirimana Blaise, Lucas Kikoti, Abed Athuman

Akiba- Adam Coast, Jamal Issa, Hamis Fakhi, Styve Nzimagasabo, John Mbise, Frank Mkumbo, George Makang'a

Advertisement