Kagere apiga mbili, Rwanda yaichakaza Shelisheli wiki

Muktasari:

Rwanda sasa inatinga hatua ya makundi kuwania kufuzu Fainali za Kombe la Dunia nchini Qatar wakiifunga Shelisheli kwa jumla ya mabao 10-0

Dar esSalaam.Mshambuliaji wa Simba, Meddie Kagere amefunga mabao mawili wakiiongoza timu ya Taifa ya Rwanda 'The Amavubi' imetinga hatua ya makundi kuwania nafasi ya kucheza Fainali za Kombe la Dunia nchini Qatar 2022 kwa ubabe baada ya kushinda 7-0 dhidi ya Shelisheli nyumbani.

Kagere alifunga mabao yake mawili kila kipindi akifunga bao moja katika ushindi huo wa kishindo wa Rwanda.

Wakati Kagere aking'aa winga wa Yanga, Patrick Sibomana amejikuta wakishangilia mabao yote 10 akiwa katika benchi alishindwa kupata nafasi ya kucheza mechi zote mbili katika kikosi cha kocha mzawa Vincent Mashami.

Mabao mengine ya Rwanda yalifungwa na kiungo Djihad Bizimana aliyefungua karamu ya mabao katika dakika 16 kabla ya Kagere kufunga bao lake la kwanza katika mchezo huo dakika ya 28, huku nahodha na mshambuliaji Jacques Tuyisenge kufunga mara mbili dakika za 29  na 34 kuifanya Rwanda kumaliza dakika 45 za kwanza kuwa mbele kwa mabao 4-0.

Katika mchezo huo uliopigwa leo usiku katika Uwanja wa Nyamirambo, Kagere alipiga bao la tano kwa Amavubi na la pili kwake katika mchezo huo dakika ya 51 huku viungo Yannick Mukunzi akipiga la sita dakika 58 kabla ya   ya Muhadjir Hakizimana ambaye ni mdogo wa Haruna Niyonzima kufunga bao la kufunga ukurasa wa ushindi dakika ya 80.

Kwa ushindi huo Rwanda wanavuka kibabe kwa jumla ya ushindi wa mabao 10-0 baada ya awali wikiendi iliyopita kutangulia kushinda ugenini kwa mabao 3-0 huku Kagere akifunga bao moja katika mchezo huo.