Kagere, Bwalya wachomoa watu Simba

Sunday September 20 2020

 

By THOMAS NG'ITU

KOCHA wa Simba, Sven Vandenbroeck amekata mzizi wa fitina dhidi yake na mshambuliaji Meddie Kagere baada ya leo kumuanzisha kwenye kikosi cha kwanza katika mchezo wao dhidi ya Biashara United.

Iko hivi, kocha Sven tangu mwishoni mwa msimu uliopita akiwa anatumia mfumo wa 4-2-3-1 alikuwa akimtumia John Bocco pekee katika eneo la ushambuliaji na kumuweka benchi Meddie Kagere.

Kurejea kwa Kagere kunamfanya John Bocco kuondolewa kabisa katika kikosi hiko huku akiwa haonekani hata katika benchi badala yake aliingia Chris Mugalu kwenye benchi.

Wakati Sven akimpa nafasi Kagere, mabadiliko mengine aliyoyafanya ni kuwaingiza kwenye kikosi cha kwanza, Pascal Wawa akichukua nafasi ya Kennedy Juma, Gerson Fraga akichukua nafasi ya Jonas Mkude na Lary Bwalya akichukua nafasi ya Benard Morrison ambaye ameanzia benchi.

Kikosi kinachoanza Aishi Manula, Shomari Kapombe, Mohamed Hussein, Josh Onyango, Pascal Wawa, Gerson Fraga, Mzamiru Yassin, Meddie Kagere, Lary Bwalya na Clatous Chama.

Katika upande wa wachezaji walioka benchi, Beno Kakolanya, David Kameta, Ame Ibrahimu, Said Ndemla, Hassan Dilunga, Chris Mugalu na Benard Morrison.

Advertisement

Kikosi cha Biashara kinachoanza; Daniel Mgore, Ally Kombo, Ramadhan Chombo, Deogratius Judika, Tariq Simba, Kelvin Idd, Mpapi Salum, Mustha Hamis, Lenny Kisu, Abdulmajid Yahaya, Omary Nassoro.

Advertisement