Jeshi Stars mabingwa wavu Nyerere cup

Timu ya Jeshi Stars imefanikiwa kutwaa ubingwa wa michuano ya kimataifa ya mchezo wa wavu yajulikanayo kama Nyerere cup.

 

Mashindano hayo yaliyofanyika katika viwanja vya Ngarenaro jijini Arusha, timu ya Jeshi Stars imefanikiwa kutwaa ubingwa huo mara baada ya kuifunga timu ya Tanzania Prison kwa jumla ya seti 3-0 katika mchezo wa fainali.

 

Akizungumzia ushindi wao nahodha wa Jeshi Stars Zainabu Thabiti alisema wamefurahi kutimiza malengo yao waliyokuja nayo katika michuano hiyo na kuahidi kuzidisha mazoezi zaidi kushiriki hadi michuano ya kimataifa.

 

"Kiukweli ni furaha ya aina yake kupata ubingwa ambao tumeupambania Sana kutokana na wapinzani wetu nao walikuwa wazuri Sana hasa wakiongozwa na kiu ya ubingwa huu"

 

Nae kocha wa Tanzania Prison, Edwin Mafinga alisema kuwa walikuwa na haja kubwa ya ubingwa lakini kwa Bahati mbaya ikashindwa kuwaangukia wao lakini hiyo haiwavunji moyo zaidi ya kwenda kujipanga kwa msimu ujao.

 

Michuano hiyo ya kimataifa yaliyoandaliwa na shirikisho la mchezo wa wavu Tanzania "Tava" yamemalizika katika viwanja vya Ngarenaro yaliyokuwa na lengo ya kumuenzi Rais wa Kwanza wa Tanzania hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.