Ibenge ‘pacha’ wa Zahera abwaga manyanga DR Congo

Muktasari:

Ibenge leo amepeleka barua ya kujiuzulu kwake katika makao makuu ya Shirikisho la soka Congo (FECOFA).

Dar es Salaam. Kocha wa timu ya taifa DR Congo, Florent Ibenge amejiondoa kufundisha kikosi hiko baada ya kupata matokeo mabovu akiwa fainali za Mataifa ya Afrika (Afcon2019).

Ibenge leo amepeleka barua ya kujiuzulu kwake katika makao makuu ya Shirikisho la soka Congo (FECOFA).

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 57, alikuwa anafundisha timu ya Taifa Congo, lakini kwa wakati huo huo alikuwa akiifundisha klabu ya AS Vita, hivyo ameona aachane na kazi moja.

Mwaka huu katika kombe la Mataifa Afrika, Congo waliondolewa katika hatua ya 16 bora na timu ya Madagascar.

Rekodi ya Ibenge akiwa na kikosi hiko aliweza kuifikisha nafasi ya tatu 2015 mashindano yaliyofanyika Equitorial Guinea, lakini pia katika hatua ya robo fainali mwaka 2017.