Huku Yanga, kule Kagera

Muktasari:

Yanga ndio timu pekee mpaka sasa kwenye Ligi Kuu Bara iliyocheza mechi chache kutokana na majukumu iliyokuwa nayo kwenye anga za kimataifa. Imecheze mechi nne na kukusanya alama saba, ikishinda mechi mbili, kupoteza moja na kuambulia pia sare moja.

ACHANA na matokeo ya jana kati ya Simba na Tanzania Prisons leo ni viwanja vitatu vinatarajia kuwaka moto ikiwa ni mwendelezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga anatarajia kuwa mgeni wa Ndanda katika uwanja wa Nagwanda Sijaona, ilihali Kagera Sugar watakuwa wageni wa KMC.


Simba ilikubali kugawana pointi moja moja na Tanzania Prisons jana  kwenye Uwanja wa Uhuru ikiwa pambano lao la kwanza kutoka sare msimu huu na pia la kwanza kuachia pointi dhidi ya maafande hao wa Magereza tangu mwaka 2012 katika mechi za nyumbani.


Ukiachana na pambano hilo ambalo litakuwa likitazamwa na wengi kutokana na timu hiyo kutoka kumtimua aliyekuwa kocha mkuu Mwinyi Zahera kutakuwa na mtihani mwingine mgumu kati ya KMC na Kagera Sugar na Azam atakuwa mwenyeji wa Biashara.


KMC inatarajia kushuka dimbani ikimkosa kocha wake mkuu kwenye benchi la ufundi huku sababu ikiwa ni kukosa vibali bvya kuendelea kufanya kazi nchini.


Huku Azam FC ikitarajia kushuka dimbani ikiwa na kumbukumbu ya kupoteza pointi mbili kwenye uwanja wao wa nyumbani baada ya kutoka sare ya bila kufungana dhidi ya Kagera Sugar.


Mkwasa leo ndio anatarajia kuanza kibarua chake cha kukaimu nafasi ya ukocha akiikabili Ndanda ambayo hawana mwenendo mzuri kwenye ligi kutokana na kutokuwa na matokeo mazuri na kujikuta inbajikusanyia pointi saba kwenye michezo nane waliyocheza.


Yanga ndio timu pekee ambayo inaingia mzunguko wa tano leo baada ya kubanwa na ratiba ya mashindano ya kimataifa na mara baada ya kutolewa kwenye mashindano hayo kwa kipigo cha bao 3-0 dhidi ya Pyramids FC sasa inahamia Ligi Kuu Bara.