Huko EPL bado kwamoto

Wednesday March 25 2020

Huko EPL bado kwamoto,LIGI Kuu England,virusi vya corona,,

 

LONDON, ENGLAND . LIGI Kuu England ambayo iko katika mapumziko ya lazima kupisha janga la kusambaa kwa virusi vya corona, inapanga kumaliza mechi zilizosalia ndani ya wiki sita tu kuanzia Juni Mosi, mwaka huu.

Msimu wa sasa wa 2019/20 umesimama hadi Aprili 30 ikiwa ni mkakati wa kudhibiti Corona, lakini ratiba mpya iliyopendekezwa na Bodi ya EPL itashuhudia msimu ujao wa 2020/21 ukianza mapema (Agosti 8), wiki nne baada ya msimu huu kumalizika.

Kama hii itafanyika, itakuwa imeziokoa klabu nyingi zinazotegemea mapato ya mlangoni na matangazo ya runinga kwani, kunahofiwa kuibuka kwa janga la kiuchumi.

Kwa mujibu wa pendekezo la Juni Mosi, ambalo limepangwa ligi kuanza, wiki 10 tu zijayo, haijapitishwa moja kwa moja lakini, inategemea uungwaji mkono wa klabu shiriki huku FA ikitaka ligi iishe.

Kama hilo litakotokea, inamaanisha vinara wa ligi hiyo, Liverpool watabeba ubingwa wao waliousubiri kwa miaka 30 sasa.

Mapema wiki hii, FA ilitangaza kuwa tayari kuongeza muda wa ligi zaidi ya Juni Mosi.

Advertisement

Kuafuatia uamuzi wa UEFA kuahirisha mashindano ya ubingwa wa Ulaya, hadi mwakani huenda mapendekezo ya kuendelea na ligi ukawa uamuzi sahihi.

Waziri Mkuu wa England, Boris Johnson, mapema wiki hii alitoa agizo la watu kukaa nyumbani ambapo vilabu, maduka, maeneo ya starehe na biashara zote kufungwa. Hakujawa na shughuli zozote za michezo Machi 13.

Advertisement