Hazard: kuichezea Real Madrid ni ndoto ya kila mchezaji

Tuesday July 10 2018

 

Moscow, Russia. Joto la mechi ya nusu fainali ya kwanza ya Kombe la Dunia 2018, itakayopigwa leo, katika dimba la St Petersburg, kuanzia saa tatu usiku, kati ya Ubelgiji na Ufaransa, nahodha wa Ubelgiji, Eden Hazard, amesema kuichezea Real Madrid ni ndoto ya kila mchezaji.

Kiungo huyo wa Chelsea, amekuwa akihusishwa na dili la kuhamia Santiago Bernabeu kujiunga na Los Blancos ambayo inakaribia kumpoteza staa wake, Cristiano Ronaldo, alitoa kauli hiyo jana, ikiwa ni mara ya kwanza tangu Madrid wane kumfuatilia.

Hazard, mwenye umri wa miaka 27,  ameiongoiza Ubelgiji kutinga hatua ya nusu fainali na kama atajiunga na Los blancos, atachukua nafasi ya Ronaldo ambaye anatajwa kuwa mbioni kutimkia Juventus. 

Kuhusu suala la kuondoka kwa Zidane klabuni hapo, Hazard ambaye anadaiwa kuwa shabiki wa Kocha huyo aliyeipa Real Madrid, ubingwa wa ligi ya mabingwa Ulaya mara tatu mfululizo, Hazard alisema hilo halimsumbui, ndoto yake iko pale pale.

"Kuondoka kwa Zidane, hakujazima ndoto zangu. kuvaa jezi nyeupe ni ndoto ya kila mtu, kwa sasa niko Chelsea, kwa sasa niko Kombe la Dunia, kitu cha muhimu kwangu ni mafanikio ya Ubelgiji," alisema Hazard.