Guinea Bissau yaita 23, mchovu Toni Silva ndani Afcon

Thursday June 13 2019

 

Cairo, Misri. Winga wa timu ya Ittihad, Toni Silva amefanikiwa kupenya katika kikosi cha mwisho cha Guinea Bissau kwa ajili ya kucheza fainali za Mataifa ya Afrika 2019, Misri.

Nyota huyo wa zamani Liverpool alijiunga na klabu hiyo ya mji wa Alexandria katika dirisha la usajili Januari, lakini alishindwa kuonyesha kiwango chache katika dakika 394, alizoichezea Ittihad msimu huu.

Katika mechi saba za Ligi Kuu Misri alizocheza, Silva amefanikiwa kutoa pasi mbili za bao dhidi ya Al Masry, na mara ya mwisho kuichezea klabu hiyo ilikuwa Aprili 2 dhidi ya Al Ahly.

Pamoja na kukosa muda wa kucheza, Silva amefanikiwa kuingia katika kikosi cha wachezaji 23 kwa ajili ya Afcon.

Atasafiri kwenda Misri pamoja na nyota wa Fulham, Marcelo Djaló, Frédéric Mendy wa Vitória Setúbal, na Mamadu Tunkara Pelé anayecheza AS Monaco.

Kipa wa UD Internacional, Edimar Vieira Cá ni mchezaji pekee wa ndani aliyeitwa katika kikosi cha mwisho cha kocha Baciro Candé, huku wengi wao wakiwa wanacheza soka Ureno.

Advertisement

Kikosi:

Makipa: Jonas Mendes (Académico Viseu), Rui Dabó (Fabril), Edimar Vieira Cá (UDIB).

Mabeki: Rudinilson Silva (Kaunas Zal), Marcelo Djaló (Fulham) Juary Soares (Mafra), Mamadú Candé (Santa Clara), Tomas Dabó (Riete), Nanú Gomes (Marítimo), Eliseu Nadjack Soares (Rio Ave).

Viungo: Sori Mané (Cova da Piedade), Mamadu Tunkara Pelé (Mónaco), Zezinho Lopes (Senica), Jorge Bura Norgueira (Aves), João Jaquité (Tondela), Moreto Cassamá (Reims).

Washambuliaji: Jorginho Intima (CSKA Sofia), Piqueti Djassi (Al Shoulla), Toni Silva (Ittihad of Alexandria), Mama Baldé (Aves), Romário Baldé (Académica), Frédéric Mendy (Vitória Setúbal), Joseph Mendes (Ajaccio).

Advertisement