Guardiola ahofia kufukuzwa Man City

Friday February 14 2020

Guardiola ahofia kufukuzwa Man City,Kocha wa Manchester Citym, Pep Guardiola,kufukuzwa,

 

London, England. Kocha wa Manchester Citym, Pep Guardiola amesema ana hofu ya kufukuzwa endapo watafungwa na Real Madrid.

Licha ya kuipa Man City ubingwa wa England mara mbili, kocha huyo ana hofu ya kutimuliwa wakifungwa katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya.

“Kama tutashindwa kuifunga Real Madrid, mwenyekiti atakuja au mkuregenzi wa ufundi atasema tunataka ubingwa wa Ulaya, naweza kukufukuza,”alisema Guardiola.

Man City imepoteza matumaini ya kutetea ubingwa mbele ya Liverpool ambayo inaongoza kwa tofauti ya pointi 22 baina yao.

Real Madrid itasafiri kwenda Etihad kuifuata Man City Februari 19 kabla ya kurudiana wiki tatu baadaye nchini Hispania.

“Ndoto yangu ni kutwaa ubingwa wa Ulaya, ingawa wapo wanasema tunacheza kwa kiwango bora na wengine wanasema hapana,”alisema Guardiola.

Advertisement

Kocha huyo wa zamani wa Barcelona na Bayern Munich, alidai matumaini yake ni kuifunga Real Madrid katika mchezo ujao na kujipanga vyema kwa mechi ya marudiano.

Advertisement