Filamu na Madrid na Neymar laja

Saturday July 14 2018

 

Madrid, Hispania. Baada ya kumaliza hekaheka za kumuondoa kundini mshambuliaji aliyewapa mafanikio makubwa katika siku za karibuni Real Madri wanageuza picha na sasa wanaanza suala la usajili wa Neymar.

Ili kuonyesha kuwa haitanii klabu hiyo imemuagiza Juni Calafat kuzungumza na baba wa mchezaji huyo ambaye pia husimama kama wakala wake.

Kwa mujibu wa Globesporte, Madrid imemtaka Calafat, ambaye ni wakala anayefanya nao kazi kuhakikisha mazungumzo yanaanza mara moja.

Madird inafahamu fika kuwa Neymar amesaini mkataba wa hadi 2022 kuitumikia Paris Saint-Germain, lakini inaamini Mwenyekiti wa klabu hiyo Nasser Al-Khelaifi atakubali kumuachiwa wakiwa na fungu la kutosha.

“Madrid inafahamu kutakuwa na mjadala mzito katika mazungumzo ya usajili wa Neymar lakini iko tayari kwa changamoto zozote zitakazojitokeza,” ilisema taarifa ya klabu hiyo.

 

Advertisement