Fan For Tomorrow yang'ara Mlimani

Saturday November 9 2019

 

By Doris Maliyaga

MASHINDANO ya Fan For Tomorrow yanaendelea kwenye viwanja vya Chuo Kikuu Dar es Salaam ambapo timu za michezo tofauti zinashiriki.
Timu hizo ni pamoja na Mlimani, Urafiki,  French,  Jerusalem, Marobo, Capstone, Egalitarian, Ardhi na Fedha.
Zinashiriki katika michezo ya soka, netiboli, basketi, riadha na rilei ambapo washindi wa kwanza wanapata medali za dhahabu, wa pili Silva na watatu shaba.
Mkurugenzi wa mashindano hayo, Albert Kimaro kutoka Kampuni ya Mobile Sports Argent amesema, lengo ni kupata burudani leo kwa ajili ya kesho.
"Mwaka huu tumefanya kwa siku moja lakini kuanzia mwakani tutafanya kwa mtindo wa ligi kama wiki moja,  tumegundua siku moja haitoshi,"alisema Kimaro.
Kimaro alifafanua, wachezaji ni wa umri chini ya miaka 11 hadi minane kwa michezo iliyotajwa.
Lakini,  wale wenye umri chini ya miaka minane, wameshiriki michezo ya fani, kuchora sura na ngongoti.
Naye, Rais wa Klabu ya Marobo FC ya Goba, Ismail Sheha alisema,  amefurahia mashindano kwa sababu vijana wanajifunza na kuendeleza vipaji vyao.

Advertisement