Fabinho amsifu Klopp kwa kumuamini

Amsterdam, Uholanzi. Fabinho amefichua jinsi kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp alivyombadilisha kuvaa viatu vya Virgil van Dijk, baada ya beki huyo wa kati kuumia goti.

Fabinho mwenye miaka 26 alikuwa na mchezo mzuri dhidi ya Ajax katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya Jumatano iliyopita, akirudishwa katika nafasi ya ulinzi wa kati akicheza pamoja na Joe Gomez.

Pamoja na kufanya ukabaji mzuri na kumakinika, Fabinho alicheza vizuri mpira uliodhaniwa kuwa bao wa Dusan Tadic katika kipindi cha kwanza na kuihakikishia Liverpool kuwa salama.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazil, ambaye kwa kawaida hucheza kama kiungo, alisema baada ya mchezo huo kuwa Klopp alimwambia kuwa mzungumzaji, hasa akiwa anacheza kama beki wa kati.

“Kiufundi, nilitakiwa kuwa tayari kwa mipira mirefu na kujaribu kuunganisha timu,” alisema alipohojiwa na Viaplay. “Haikuwa rahisi lakini nilitakiwa kufanya kidogo kati ya vile ambavyo Virgil anavyofanya kila siku, kuzungumza na timu na kuwaweka pamoja.

“Ni kweli kwamba siwezi kuiga kila kitu lakini nitajitahidi. Ilikuwa muhimu kwangu na timu kwa ajili ya kutoruhusu bao, na hiyo imenipa kujiamini.