England yapigwa nyumbani

LONDON, ENGLAND. MICHUANO ya UEFA Nations League iliendelea jana ambapo timu ya Taifa ya England ikiwa nyumbani ilikubali kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Denmark katika mchezo uliopitwa katika dimba la Wembley.

 

Matokeo hayo yanaifanya England kushuka katika msimamo wa kundi B ambapo sasa inashika nafasi ya tatu  ikiwa imepoteza mchezo mmoja, sare moja na kushinda mechi mbili ikiwa na jumla ya alama saba, huku Denmark ikipanda hadi nafasi ya pili ikiwa na alama saba pia.

 

Kocha wa England, Gareth Southgate alisema moja ya sababu ambazo ziliwafanya kupoteza mchezo huo ni kadi nyekundi ya mapema aliyopata beki wake Harry Maguire dakika 31.

 

"Ilikuwa ngumu kucheza na wachezaji kumi, mipango yetu mingi iliharibika, lakini nipongeze kile kilichofanywa na safu ya ulinzi kwa kuwa ilizua kwa umakini mkubwa, Grealish hakucheza kwa sababu nilihitaji kasi zaidi hasa katika eneo la pembeni,"alisema.

 

Mchezo mwingine mkali ulikuwa kati ya Italia na Uholanzi ambao ulimalizika kwa sare ya bao 1-1, ambapo lile la Italia lilifungwa na Lorenzo Pellegrini na lile la Uholanzi likafungwa na Donny van de Beek.

 

Matokeo ya mechi nyingine

 

Poland 3 - 0 Bosnia and Herzegovina

 

Iceland 1-2 Ubelgiji

 

Croatia 1 - 2 Ufaransa

 

Ureno 3 - 0 Sweden

 

Norway 1 - 0 Northern Ireland

 

Romania 0 - 1 Austria

 

Scotland 1 - 0 Czech Republic

 

Slovakia 2 - 3 Israel

 

Russia 0 - 0 Hungary

 

Uturuki 2 - 2 Serbia

 

Finland 1 - 0 Ireland

 

Bulgaria 0 - 1 Wales

 

Estonia 1 - 1 Armenia

 

North Macedonia 1 - 1 Georgia

 

Ugiriki 0 - 0 Kosovo

 

Moldova 0 - 4 Slovenia

 

Lithuania 0 - 0 Albania

 

Belarus 2 - 0 Kazakhstan