Emery aaambiwa atafute mabeki wa kazi Arsenal

Muktasari:

  • Nicholas alisema Emery hapaswi kutumia mude mrefu sana katika kutafuta wachezaji wa kuja kuchukua nafasi za mabeki wa kati Laurent Kosicleny na Shkodran Mustafi.

London, England. GWIJI wa Arsenal, Charlie Nicholas amemwambia kocha Unai Emery kwamba anapaswa kufanya usajili wa mastaa wapya haraka iwezekanavyo.

Wakali hao wa Emirates bado hawajafanya usajili wowote hadi sasa huku dirisha la usajili wa majira ya kiangazi siku zikizidi kwenda ambapo rimu nyingine zimekuwa zikijiimarisha zaidi.

Staa huyo wa zamani wa Arsenal, Nicholas alisema Emery hapaswi kutumia mude mrefu sana katika kutafuta wachezaji wa kuja kuchukua nafasi za mabeki wa kati Laurent Kosicleny na Shkodran Mustafi.

"Asajili mabeki wawili wa kati haraka sana," alisema na kuongeza.

"Mabeki wanahitajika haraka. Wanapaswa kuja mapema ili kuendana na kasi ya timu kwa sababu wakichelewa itakuwa shida.

"Beki aliyekuwa na kasi alikuwa Koscielny, lakini sasa amekwisha, hivyo wanahitaji mabeki wenngine wa kati wenye kasi zaidi. Mabeki hao walikuwa vizuri kipindi cha Arsene Wenger. Wameharibiwa na majeruhi, si makosa yao."

Kumekuwa na ripoti kwamba beki Koscielny anafikiria mpango wa kuachana na timu hiyo na kurudi zake Ufaransa, huku Mustafi akitajwa kuwa mmoja wa wachezaji ambao kocha Emery anataka kuwauza ili kupata pesa za kunasa nyota wapya anaowahitaji.